BARIADI-MKOA MPYA WA SIMIYU.

Safari yangu ikanifikisha Bariadi mjini kwenye msiba wa mmoja wa mama zangu. Bahati ikawa upande wetu, mimi na bi mkubwa wangu, tukawahi siku ya mazishi. Kwa hakika siku hiyo nyumbani kwa baba; Mzee Juma Seif Nguzo (mzee wa Kiluguru) palikuwa pamefurika vilivyo idadi kubwa ya watu; ndugu, jamaa na marafiki wa Bariadi na kutoka pande nyingine mbalimbali za nchi. Ilikuwa ni siku ya huzuni kubwa. Bahati nzuri shughuli yote ya mazishi ilikwenda vizuri; marehemu akasitiriwa vema kwenye makaburi yaliyopo eneo la Kidinda-Bariadi mjini. 

 

      Bariadi kuna vijimambo, wakwetu! Hebu ngoja nianze kukupa polepole kwa kuanzia hapa....

 

Na hii ikawa ni siku ya pili na ya tatu tangu mwili wa marehemu ulipozikwa.

Waliokaa mbele wakijadiliana jambo juu ya simu waliyoishika ni Malima Mtesigwa (mwenye shati jeupe) na Siki Manuali (mwenye shati jekundu). Wanaowatazama kwa nyuma ni mwalimu Munyu Lyamtema (mwenye shati la mistari ya bluu) na Musiba Mtesigwa.

 

Mwenye fimbo katikati ni mwalimu Msakambi 'Sosi' wa shule ya msingi Mugango-Musoma akielekezana jambo kwenye simu na mmoja wa wazee maarufu wa Bariadi aliyejiinamia, Babu Mzee Mkoyongi. Anayewatazama kwa makini ni Matata Inos 'mzee wa vizingani', mmoja wa watoto wa marehemu.



 Kutoka kushoto ni Magai Muyabi, Andrew Mtesigwa (katikati) na John Muyabi.

 


Aliyetabasamu ni Malima Mtesigwa, Fikiri Juma (mmoja wa watoto wa marehemu) na Siki Manuali (mwenye shati jekundu)



 Mwenye kofia nyeupe aliyeshika goti ni Salum Mkoyongi 'mzee wa machimboni-Geita'



Jicho kwenye kamera ni mzee mwingine maarufu wa Mji wa Bariadi, Babu Mzee Mapesa.



Aliyekaa akiwa ameshika kidevu ni Majeshi Mtesigwa 'mzee wa machimboni', akiwa amezungukwa na ndugu na jamaa wa marehemu. Huyu bwana mkubwa ni mmoja wa vijana waliolelewa kwa muda mrefu na marehemu.



Ukitaka kukosana na kibogoyo, wewe jaribu tu kumpa vitu kama hivi walivyokamatia hawa jamaa! Aisee hii ni hatari! Unaweza hata ukang'oka jino kwa uhondo wa mfupa! Kutoka kushoto wakishughulika vilivyo, ni Matata Inos, Malima Mtesigwa na Andrew Mtesigwa. 



Hapa tunavuta pumzi kidogo na kutazama kwa makini ni sehemu gani yenye kajimnofu inayofaa kupigwa jino kwenye hili jimfupa. 

 


Dogo naye hakuwa nyuma katika kujituma. Mikono yote miwili inapiga kazi kama kawa. Anaitwa Anko Juma.

 

 

Shika hii. Aah! Wapi, wewe! Kumbe ujanja wake wote dogo analiogopa ile mbaya kongoro (kwato) la ng'ombe! Hapa ilikuwa ni almanusuru akimbie! Kamata pisto hiyo, dogo ujibwede!



 Aisee, jamaa wachokozi hawa! Hivi wana mpango gani hasa na huyu dogo hata waamue kumpa huu mtanange mkubwa namna hii ili ajipime nao ubavu! Nahisi wanataka ajing'oe bure vijimeno vyake vya utoto. 



No comments: