UDAKU-ARUSHA. Kuwa Makini!



Vyovyote itakavyokuwa, lakini wiki hii katika mtaa maarufu wa Jamhuri mjini Arusha-kata ya Daraja mbili pametokea kali ya aina yake. Mambo ya facebook bwana! Kwamba wawili fulani (mwanamke na mwanamume) waliwasiliana kwa muda mrefu kupitia mtandao wa facebook bila ya kufahamiana wala kukutana. Basi, siku ya siku wakaamua watafutane; bahati nzuri wakakutana mjini Arusha; wakaamua wale raha kwa vinywaji na mapochopocho kedekede. Kama unavyoelewa tena kilevi cha aina yoyote ile kimeonywa sana kila mahali katika maandiko matakatifu kwamba ni baba wa maasi. Kilevi kilipowakolea, wawili hawa wakaamua wajichukulie chumba kwa mapumziko kwenye gesti moja maarufu katika mtaa wa Jamhuri. Ndipo ghafla tu, lahaula, usiku mwanamke akakurupuka mbio kutoka chumbani akiwa full naked (hana kivazi chochote kile mwilini; yaani mtupu kabisa) akipiga mayowe ovyo kwamba mwenza wake chumbani amegeuka mnyama Chui na kuanza kumparura mwilini (akawa anaonesha mikwaruzo). Mmoja wa wahudumu wa gesti hiyo anadai wakati mwanamke huyo alipokurupuka, yeye alitupia jicho kwa chati kwenye chumba hicho wakati mlango ukiwa wazi naye akamwona mnyama Leopard! Kundi la watu lilipojikusanya likaamua kwenda kwenye chumba hicho chenye Chui-mtu, na kumkuta huyo bwana amepozi tu kitandani akiwa ni binadamu wa kawaida! Mwanamke akagoma kabisa kurudi ndani ya chumba hicho; ikambidi alale hadi asubuhi na wahudumu wa gesti. Asubuhi jamaa 'chui-mtu' akalipia chumba na kutambaa zake kivyake mbele kwa mbele!  Wewe unaionaje hii? Kazi ni kwako.

No comments: