Ni muda wa kama saa sita kasoro dakika kadhaa hivi za
mchana Mjini Arusha. Huu ni moja ya misururu mirefu (msongamano wa magari)
katika barabara maarufu ya Sokoine, eneo la Metropole. Kama siku mbili tatu
hivi, nahodha wako nilikuwa ndani ya jiji la Dar es salaam katika pilikapilika
zangu hizi na zile. Katika moja ya vitu vinavyowaumiza sana vichwa wakazi wa
jiji hilo kubwa, ni hali ya msongamano mkubwa wa magari (jam), iwe ni kwa
usafiri wa binafsi au kwa Daladala, hali ni moja tu. Wakati mwingine unaweza
ukawa unakwenda eneo la karibu tu kutoka pale unapoishi, lakini kama wewe ni
mgeni kabisa katika jiji hilo, basi unaweza ukafikiri umekwenda eneo la mbali
mno! Kama wewe ni mwenyeji wa jiji hilo japo kidogo, hebu pima umbali wa kutoka
stendi kuu ya mabasi-Ubungo hadi kona ya kuingia barabara ya Shekilango ili
uelekee pande za kwa wajanja (Sinza) hadi Mwenge au Tandale kwa Tumbo na Kinondoni!
Mbona ni karibu tu. Lakini hebu ujikute umenasa sasa ndani ya huo msongamano wa
magari! Unaweza ukafikiri ni mbali kupita kiasi, kumbe wapi bwana! Dalili ya Mji
wa Arusha nayo imeanza polepole kufanana na ya Jiji la Dar es salaam. Hebu jionee
mwenyewe.
|
No comments:
Post a Comment