JIKONI NAKO, MAANDALIZI NA MAPISHI YALIKUWA MOTOMOTO.

 Tulieni ninyi niwaoneshe maufundi na mavituuuuz yangu ndani ya hili sufuria. Mwanafunzi wa kidato cha 4, Pendo Kimolea, aliyekamatia mwiko, akiwa kazini, kuhakikisha kwamba mambo ya mlo yanakuwa bambam. Hawa, wao waliamua kuwaunga mkono wahitimu wenzao wa dini ya kiislamu.



 Leo, nitahakikisha wanakula hadi wenyewe waseme basi. Mwanafunzi wa kidato cha 4, Anita, akiwa kazini jikoni.



Hapa ni tabasamu na kazi tu kwa kwenda mbele. Hivi vitunguu vyote navishughulikia harakaharaka ili viingie jikoni. Mwanafunzi wa kidato cha 4, Magdalena Lodrick, naye alichacharika vilivyo.


Hebu ngoja nionje kidogo kama mambo yameshakuwa tayari. Uhondo mtupu. Mwanafunzi wa kidato cha 4, Janeth Peter, ndani ya sura ya madikodiko na mahanjumati.

No comments: