LIKAFUATA ZOEZI TAMU. HAPA ILIKUWEPO KEKI 1 TU ILIYOKUWA IMEANDALIWA NA WAHITIMU. KWA HIVYO, KILA MHITIMU ALITAKIWA ALISHWE KIPANDE 1 NA MZAZI AU MLEZI WAKE. NDIPO WAKAJIMWAGA JUKWAANI! ZILIKUWEPO PICHA NYINGI TU TAMU. LAKINI HIZI CHACHE ZILIUVUTIA ZAIDI Mpini Wa Shoka.

 Jamani, baba! Mbona umechukua kipande kikubwa namna hii! Nitaweza kweli kukimeza? Mzazi Hamza Hassan akimlisha keki binti yake, Mariam Hamza, ambaye yeye mwenyewe (Mariam) ndiye aliyeiandaa keki hii kwa niaba ya wahitimu wenzake wote wa kiislamu wa kidato cha 4.



 Hiki ni kikubwa sana? Acha masihara wewe. Hiki utakimeza tu bila ya wasiwasi wowote. Mbona wakati ule ulipokuwa bado kaduuuchu (mdogo) nilikuwa nakulisha matonge makubwa tu ya wali kuliko hata ukubwa wa hiki kipande cha keki, na ulikuwa unayameza vizuri tu! Au siku hizi mdomo wako umekuwa mdogo? Hebu fungua mdomo, usiniletee porojo hapa.



Kwa mwendo huu, mbona mwenzenu nitanyongwa na hili jipande la keki, jamani? Khadija Saidi Kivuyo akilishwa keki na mwanafamilia wake, Mama Saadi.

No comments: