MASHINDANO NA MICHEZO KADHAA KWA AJILI YA KUMKARIBISHA MGENI RASMI IKAANZA.


 Kufukuza upepo nako kulikuwepo. Shuhudia mwenyewe. Hapa mwanafunzi Nice Emanuel akitifua vumbi katika mashindano ya mbio za vijiti 

 

 Hapa napo ni katika mashindano ya mbio kutoka goli moja la uwanja hadi jingine! Hiki ni kituko! Hizi mbio mwanawane, zilikuwa ni kwa wawili wawili wanaunganishwa mguu mmoja mmoja kwa kufungwa na kamba, halafu kazi ya kutimua mbio inaanza! Mwee!




Hawa walikuwa katika shindano la kujaza maji kwenye chupa. Nalo pia lilikuwa ni sawa na shindano la mbio tu, kwani ndoo za maji zilikuwa mbali sana, kwa hivyo hapa ilikuwa ni kukimbilia kwenye ndo kuchota maji na kuja kujaza chupa. Vitoto vvenyewe vidooooooogo, maji hata hayalengi vizuri mdomo wa chupa!

 

 Hivi viatu siyo kwamba vilikuwa vimetupwa tu! Hapana. Hili nalo lilikuwa ni shindano jingine. Yaani wenye viatu hivi, kwanza kila mmoja alitakiwa avitambue viatu vyake, kisha avivae kwa haraka bila ya kukosea. Hapo ndipo visa na mikasa vikaanza! Tazama hapa chini. 

 

Jamani, mbona hiki hakiingi! Au Siyo cha kwangu! Hebu ngoja nikushike bega mshiriki mwenzangu, labda kitakubali kuingia!


Mimi hata sielewielewi! Ngoja nisimame kidogo nimwangalie huyu dada naniii yeye anavaaje, halafu na mimi ndio nianze kuvaa vya kwangu! 

 


Cheka unenepe! Huyu kweli ndiye aliyekuwa wa kwanza kabisa kuvaa viatu, lakini hakushinda! Ni kwa sababu gani! Hebu mkague vizuri miguuni.



HALAFU LIKAJA SHINDANO LA KUVAA SHATI KWA HARAKA! VILIKUWA NI VITUKO VITUPU! UNAFIKIRI NI NANI HASA HAPA CHINI ALIYEIBUKA MSHINDI? HAPA ILIKUWA SHUGHULI NZITO! WAZAZI NA WALEZI, NAJUA MNAWAPENDA SANA WATOTO WENU, HASA VIDOGODOGO KAMA HIVI, LAKINI MSIWAFANYIE KILA KITU NYAKATI ZOTE. WAKATI MWINGINE WAAMBIENI WAJIFANYIE WENYEWE.

Hata sijui mkono wa hili shati uko wapi sasa! Mwanafunzi Saadi Abdillahi akijitahidi kupambana na wenzake katika shindano.



Huyu sasa yeye ndio amelivaaje hili shati lake (aliyekupa mgongo)! Ndio tayari amemaliza kazi!

No comments: