WAKATI WA MGENI RASMI UKAFIKA.


Mgeni rasmi, Mussa Maalim, akisisitiza jambo. Kwa umri kwa hakika anaonekana bado ni kijana mdogo mno. Lakini maneno na wosia alioutoa kwa wahitimu, wazazi pamoja na walezi wote waliohudhuria katika maafali haya, kwa hakika ulikuwa ni mzito mno, na hasa katika suala la maadili na kujinasibisha (kujifananisha) katika maisha, hasa kimavazi na kitabia, na watu ambao waziwazi wamekwishajitangaza na wakati mwingine kujiandika kwenye miili yao kwamba wao ni washirika wa shetani, na amri pamoja na maamrisho ya Mwenyeezi Mungu wao hayawahusu kamwe! Ulikuwa ni ujumbe mzito akinukuu vifungu na aya kadhaa kutoka kwenye kwenye biblia na Quran tukufu. 

No comments: