BARIADI MJINI
Kwa siku nilizokuwepo Bariadi, kwa hakika kila siku sikuacha kupitapita hapa na pale....Na moja ya sifa kubwa zilizonivutia sana katika Mji huu, ni mpangilio wake wa kuvutia wa mitaa. Hakuna vichochoro visivyo na macho wala miguu hapa kama ilivyo mfano wa jiji la Arusha, ambalo idadi ya vichochoro vyake vya hatari ni kubwa mno kuliko idadi ya barabara na mitaa! Kwa hakika, Bariadi panapendeza sana. Hongereni sana....
Moja ya mabango yanayoelekeza kwenye barabara kuu ya Lamadi-Bariadi-Maswa-Shinyanga. Ukipotea, ni wewe mwenyewe umejitakia.
Kwenye barabara kuu ya Lamadi-Bariadi-Maswa-Shinyanga; Pikipiki maarufu kama bodaboda zipo kibao, lakini bodaboda za jadi (Baiskeli) nazo pia bado zipo uwanjani, na zinaendelea kupiga kazi kama kawaida. Si unamwona mwana mama huyu hapa pembeni kushoto anavyojiandaa kupanda kwenye bodaboda ya jadi!
Co-operative and Rural Development Bank (CRDB), makao makuu mkoa mpya wa Simiyu, mjini Bariadi.
Hapa ni katikati ya Mji wa Bariadi kwenye stendi kubwa ya zamani ambayo kwa sasa imehamishiwa nje kidogo ya Mji; nikakutana na shindano hili. Wakwetu, hapa mshindi hakupatikana kwa sababu ya kumaliza haraka, hapana. Palikuwa na vigezo na masharti. Na majaji ni wananchi wenyewe waliokuwa wakishuhudia. Kwa hivyo, majaji walitakiwa wakodoe macho yao kwa makini kabisa, ili yule atakayetimiza vigezo na masharti kwa usahihi ndiye wamchague. Sharti la 1:- ukianza kunywa, hakuna kushusha chini chupa hadi umalize kabisa. Kigezo cha 2:- wakati unaendelea kunywa, soda isichuruzike hata kidogo na kutokea pembeni mwa mdomo. Sharti la 3:- hakuna kutapika jukwaani! Sharti la 4:- ukimaliza kunywa, hakuna kufuta mdomo ili kupoteza ushahidi wa sharti(kigezo) namba 2. Na mwisho:- ukimaliza kunywa, weka chupa yako tupu kichwani ili majaji wahakikishe kwamba kweli umemaliza. Basi ajabu na kweli, aliyemaliza wa mwisho (wa kwanza kushoto kabisa) ndiye aliyeibuka mshindi, na kujizolea zawadi ya soda zingine kadhaa za kuendelea kujipongeza zaidi!
Mji wa Bariadi kama ilivyo miji mingine, nako pia majengo ya ibada hayakosekani; Makanisa kwa Misikiti. Huu ni mmojawapo wa misikiti iliyopo katika Mji huu kwenye barabara kuu ya Bariadi-Shinyanga. Hapa kwa siku za nyuma ulikuwepo msikiti wa kawaida tu wa mbao. Lakini sasa waumini wameubadili kabisa kama unavyoonekana.
Hapa ni kwa ndani ya Msikiti huo.
Miongoni mwa vionjo vya Mji wa Bariadi, ni vitu kama hivi. Vitu vya nguvu. Kila mtaa unakopita ni lazima utakutana navyo tu. Wakwetu, kamji kanapendeza ile mbaya.
No comments:
Post a Comment