HOME-ARUSHA

Nilipofika nyumbani Arusha baada ya safari na mizunguko mirefu ya huku na huko, nilipumzika kidogo kisha nikaelekea kuwaona wanafamilia wangu nyumbani kwa bibi yao, maeneo ya Njiro. Wakwetu, wanafamilia wangu walifurahi sana kuniona, hasa yule mdogo kabisa ambaye alinifanyia kila aina ya kituko....


 

Alinipigia makofi na kunichezea vitu vingine hata sikuvielewa kabisa





 

Pia alinionesha ni kwa namna gani na yeye anataka sasa aanze kwenda shule kama wenzake, baada ya kung'ang'ania avalishwe mgongoni begi la shule la dada yake; halafu akaanza kupiga hodi kwenye mlango wa gari ili apakizwe apelekwe shule! Sasa sijui huko shuleni akipelekwa ataelewana vipi na walimu pamoja na wanafunzi wenzake, wakati hata kuongea lugha yoyote ile inayoeleweka bado hajui kabisa! 






Hawa ndio wakubwa zake na raha zao.





Hapa wanajaribu kumsaidia kumshika mikono na kumtembeza; lakini kawaida yake huwa hataki kabisa mtu yeyote yule amshike mikono na kumtembeza! Anataka atembee yeye mwenyewe tu, hata kama akianguka chini mara saba.



 

 

---lakini wiki hii, mimi na mke wangu tumekuwa katika unyonge kidogo. Binti yetu mkubwa (huyo aliyemshika mkono mdogo wake), alikuwa na matatizo kidogo ya maumivu ya tumbo; akajikuta akifanyiwa oparesheni ya kitovu. Any way, nitakutupia tu mbili tatu za hospitalini. Kwa sasa bado yuko wodini na mama yake. Dah! Wakwetu, hata mimi ninao moyo na roho sawa tu na vile ulivyo wewe. Kwa hakika, nilipatwa na hofu nyingi; lakini namshukuru mno Mwenyezi Mungu kwa mapenzi yake makubwa...



No comments: