BUSTANI ZA MITI NA MAUA

Wakati kikundi cha vijana wa mwanzo kabisa kuanzisha wazo la mpango wa kuweka vitalu vya miche ya miti pamoja na maua pembezoni mwa barabara maarufu ya Phillips jijini Arusha, wengi wetu tuliwaona kama vile ni wendawazimu tu wasiokuwa na lolote lile la maana! Lakini baada ya miaka kadhaa sasa, wazo hili limeenea vema kote katika jiji hili. Pembezoni mwa barabara nyingi kubwa pameonekana kupendeza na kuvutia sana kwa bustani za miche ya miti pamoja na maua ya aina mbalimbali. Kwa hakika, kila jambo zuri linahitaji subira na uvumilivu wa dhati kutoka moyoni ili kulifikia lengo lililokusudiwa....Mpini Wa Shoka ulipitisha jicho katika bustani hii kongwe (bustani anzilishi) iliyopo pembezoni mwa barabara ya Phillips

Wengi wanaoendesha kazi hii, hasa vijana, kwa hakika wameweza kujikimu vilivyo kimaisha ndani ya jiji la Arusha..

No comments: