ELIMU HUANZIA NYUMBANI!

Ingawa shuleni ndiko hasa kunakopatikana maarifa makubwa ya kielimu, lakini chachu na chachandu ya kuyafikia vema maarifa hayo huanzia na hamasa pamoja na msukumo kutoka nyumbani. Je, mimi na wewe, kati yetu ni wangapi tunaowapa nafasi watoto wetu kuanza kujifunza nyumbani taratibu hata kama bado hawajaanza rasmi kwenda shuleni? Au hata sisi wenyewe kukaa nao japo kwa dakika 5 tu ili kuwapa hamu na msukumo wa kuyapenda masomo! Au kazi yetu kubwa ni kuifungulia tu midomo na kuzisukumiza lawama kedekede kwa walimu, mashule na Serikali baada ya watoto wetu kuchora Zombi (karagosi) na beti za nyimbo kwenye karatasi zao za mitihani na kuambulia vibuyu (Zero)!

Saadi Abdillahi akijaribu kufanya zoezi alilopewa na dada yake nyumbani




Huyu ni Bi. Shadya; naye pia akijaribu kufanya zoezi alilopewa na dada yake nyumbani. Baada ya hapa kazi ni moja tu; kucheza na baiskeli mtindo mmoja.

 




No comments: