KIKOSIKAZI CHA WANA MtuKwao; KUTOKA MTWARA-KUSINI MWA TANZANIA CHATUA KATIKA MJI MDOGO WA TERRAT ULIOPO WILAYANI SIMANJIRO; MANYARA-KASKAZINI MWA TANZANIA...


Ni katika ziara ya siku moja ya mafunzo iliyofanyika siku ya Jumanne ya tarehe 20/08/2013. Shirika lisilo la kiserikali la MtuKwao lenye kuihudumia zaidi mikoa ya Lindi na Mtwara, lipo mbioni kuanza kurusha matangazo ya redio yake mpya inayotarajiwa kufunguliwa wakati wowote ule katika eneo la Naliendele-nje kidogo ya Mji wa Mtwara. Wakati wakijiandaa kwa ufunguzi huo, Wana MtuKwao wamekuwa wakijaribu kufanya ziara kadhaa za mafunzo ya kujiandaa, ambapo wamewahi pia kukitembelea kituo cha redio Pangani Fm kilichopo mkoani Tanga. Sasa ziara yao imewafikisha Simanjiro mkoani Manyara kwenye Shirika la Ilaramatak Lorkonerei lenye shughuli mbalimbali mchanganyiko za kijamii, ikiwemo redio maarufu ya O.R.S FM (Orkonerei Radio Service.) Mpini Wa Shoka ulikuwepo ndani ya ziara hii...


Hapa kikosi cha wana MtuKwao kikiwa kimepokelewa kwa maelezo ya mwanzo kutoka kwa program officer wa ORMAME-Orkonerei Mass Media, Bw. Lucas Abraham Ole Kariongi (aliyesogezewa kinasa sauti), ambayo ndiyo inayosimamia kituo cha redio ndani ya shirika la Ilaramatak.




  

Mzunguko wao ukaanzia kwenye kiwanda cha kusindika bidhaa zitokanazo na maziwa...



Kiongozi wa msafara huu wa Wana MtuKwao, ambaye pia ndiye mkurugenzi wa Shirika hilo, Bw. Swallah Saidi Swallah, akiweka saini yake kwenye kitabu cha wageni kwenye ofisi ya meneja wa kiwanda cha maziwa





Meneja wa Kiwanda cha maziwa-Terrat, Bi. Nasinyari Marco aliyewapokea na kuwapa maelezo na majibu kadhaa ya maswali yao...




Baada ya mazungumzo na meneja wa kiwanda, wakapata fursa ya kuingia ndani ya kiwanda chenyewe cha maziwa..



Wakivaa mabuti maalumu ya kuingilia ndani ya kiwanda...




Pamoja na mabuti maalumu, pia wakavalia kama unavyowaona wakiwa na dada anayehusika na shughuli za ndani ya kiwanda...





Nje ya kiwanda wakapata picha ya pamoja...




Mzunguko wao ukawafikisha kwenye idara ya Video iliyo chini ya Ormame-Orkonerei Mass Media...




Kiongozi wa idara hiyo, Bw. Edward Phillipo Ole Koreiya, (mwenye shati jeupe la mistari-picha juu) akiwapa maelezo. Picha chini na juu wana MtuKwao wakiwa wamemzunguka wakimsikiliza kwa makini na kunukuu kwenye vitabu vyao...




Pamoja na maeneo mengine, hatimaye wana MtuKwao wakafika ndani ya studio ya kurushia matangazo ya kituo cha redio ya jamii cha O.R.S FM (Orkonerei Radio Service) Terrat-Simanjiro...



Mtangazaji wa zamu, Salome, (aliyekaa) akiendelea na kipindi chake. Mwenye shati la rangi ya bluu nyuma yake ni meneja wa kituo Bw. Baraka David Ole Maika. Aliyekunja mikono kulia ni Mohamed Massanga wa wana MtuKwao-Mtwara




Kiongozi wa msafara wa wana MtuKwao, Bw. Swallah Saidi Swallah (aliyekaa), akapata nafasi ya kuhojiwa hewani moja kwa moja juu ya masuala kadhaa, yakiwemo malengo ya ziara yao hii...





Vijana wake wakiwa wametulia wakimfuatilia. Kutoka kushoto kabisa ni Shafih Ndege, Gregory Millanzi, Issa Hemedi, Mohamed Massanga. Mwenye shati jeupe ni production manager na mtangazaji wa O.R.S FM-Wilbard Kiwale 'Kiwa4life'. Kulia kabisa ni Salehe Kaondo wa MtuKwao.





Mpini Wa Shoka (katikati-mikono mfukoni) nao ukapata picha moja pamoja na Salehe Kaondo (kushoto), program officer wa ORMAME-Orkonerei Mass Media (anayefuata kushoto). Kulia mwenye daftari mkononi ni Gregory Millanzi. Na kulia kabisa ni Issa Hemedi 'mzee wa IT'




 

Kisha wana MtuKwao wakapata fursa ya kuzungumza moja kwa moja na mwanzilishi wa Shirika hili la Ilaramatak Lorkonerei...

 Bw. Martin Saning'o Ole Kariongi-Mkurugenzi wa Ilaramatak akiwafafanulia jambo wana MtuKwao....

 

 

Mkurugenzi wa MtuKwao, Bw. Swallah Saidi Swallah, akibadilishana mazungumzo na Bw. Martin Saning'o Ole Kariongi

 



Baadhi ya vijana wa MtuKwao-Mtwara, kuanzia kushoto: Salehe Kaondo, Mohamed Massanga (kati) na Gregory Millanzi, wakiyafuatilia kwa makini mazungumzo ya wakubwa hawa wawili...





Halafu ziara ikahitimishwa kwa picha maridadi ya pamoja kutoka kwa Mpini Wa Shoka....



Waliosimama kutoka kushoto ni program officer wa Ormame-Orkonerei Mass Media Bw. Lucas Kariongi, Mohamed Massanga, Issa Hemedi 'mzee wa IT, Gregory Millanzi na Salehe Kaondo. Waliokaa ni Bw. Martin Saning'o Ole Kariongi-Mkurugenzi wa Ilaramatak Lorkonere Terrat Simanjiro (Kushoto) na Bw. Swallah Saidi Swallah-Mkurugenzi wa MtuKwao Mtwara

  



Mwenye shati la viboksiboksi (draft bluu na nyekundu waliosimama), ni Shafih Ndege-Producer wa Video-MtuKwao





Mojawapo ya picha maridadi kabisa za mwishomwisho. Hapa wakiwa pamoja na Meneja Msimamizi na Huduma wa kituo cha Ilaramatak Lorkonerei, (center Manager) Bi. Flora Gerald Lyimo (katikati), kabla hawajaingia rasmi ndani ya gari na kurejea jijini Arusha...



"asubuhi na mapema ya tarehe 21/08/2013- Wana MtuKwao wameondoka kurejea nyumbani Mtwara kupitia Dar es Salaam"







No comments: