Ebwana eeee! HUYU NI KINYONGA, AU NI KENGE mla mayai!


Wakwetu, niwie radhi sana. Hii stori niliisahau kabisa kukutupia mapema. Lakini any way, nilipokuwa katika kijiji cha Naliendele mkoani Mtwara hivi karibuni, nilikutana uso kwa uso na kinyonga huyu. Ukubwa wake ndio hasa ulionishitua sana. Siku zote maishani mwangu nimezoea kuwaona na kukutana sehemu mbalimbali na vinyonga wenye maumbile na ukubwa wa wastani tu, na wala kamwe sikuwahi kukutana na jidude kubwa kama hili..! Hebu niambie, je wewe katika pitapita zako za huku na kule ulishawahi kukutana na kinyonga mwenye ukubwa wa sampuli hii? hatari!   



Hapa alikuwa akijaribu kupanda juu ya mnazi. Wenyeji wa kijiji hiki cha Naliendele walinidokeza kwamba kinyonga huyu alikuwa ni mjamzito; kwa hivyo, alikuwa anakwenda juu kabisa ya kilele cha mnazi huu ili akajiachie hadi chini; apasuke ili watoto waliomo tumboni watoke! Hey! Eti ni kweli hivyo ndivyo vinyonga huwa wanajifungua ujauzito wao?

No comments: