HATA HAPA PIA NI NDANI YA DAR ES SALAAM. HAUNIAMINI!

 

Mpini Wa Shoka ndani ya Kibamba Kwa Mangi-Bongo! Ni eneo lililopo baada ya kutoka Mbezi kama unaelekea mkoa wa Morogoro au Arusha na Moshi ukitokea Dar kwa barabara kuu.

Ndani ya huu msitu kuna nyumba kalikali tu (nzuri). Baadhi zimekwishahamiwa na wenyewe au kupangishwa; na nyingine ndio kwanza bado zimo katika ujenzi.




Hii ni mojawapo ya nyumba hizo. Hii hata haijahamiwa. Wakwetu, nikufanyie mpango?





Barabara na mitaa ya sampuli hii kwa Kibamba ni ya kawaida tu! Si unawaona wenyeji wanadunda bila ya wasiwasi wowote! Sasa sijui kama hawa wawili  walikuwa pamoja wakiongozana, au kila mmoja alikuwa na hamsini zake..! Miye simo! 





Misitu na mabonde kama hivi kwa Kibamba navyo pia ni vitu vya kawaida tu. Kiukweli, panavutia.




Madaraja ya mbao kama hili Mpini Wa Shoka uliyashuhudia hapa na pale. Wenyewe wenyeji wanakwambia, hapa hata lori kubwa la mchanga ama kokoto linapita tu bila ya wasiwasi wowote ule..! Ha!





Bodaboda kama kawa kila upande. Hata mimi pia nililetwa na moja kama hii kupitia kwenye daraja hili hadi nyumba kwa sister'angu mmoja anayeishi na familia yake ndani ya Kibamba hii ya Kwa Mangi-Dar es Salaam


No comments: