Kwa jina maarufu anafahamika zaidi kama 'Mapinduzi'...

...ni mkazi wa Kijiji cha Nguruma, Kata ya Akeri, Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha. Jina lake halisi ni Humphrey Kaaya.  Mpini Wa Shoka ulimtembelea nyumbani kwake pande za Nguruma na kujionea mambo chungu wa tele. Aisee! Sielewi hata nimwite mkulima! Mfugaji! Ama kwa jumla nimwite mjasilia nguvu na akili..!  

Hapa amepouz pembeni mwa shamba la migomba...



Hapa akijaribu kunifafanulia jambo fulani kwa kuchora chini pembezoni mwa mdomo wa kutolea kinyesi cha mifugo kwenye mtambo wa gesi...




Hizi ni chemba za kumiminia kinyesi cha mifugo kwenye mtambo wa gesi...


  


Huu ndio mtambo wenyewe wa gesi ambao ulijengwa na wa taalamu kutoka CamaTeq (Arusha) mwaka 2012... 



Hawa ni baadhi ya ng'ombe ambao ndio chanzo kikuu cha malighafi (kinyesi) kwa ajili ya mtambo wa gesi, gesi ambayo inaisaidia familia kwa matumizi mbalimbali na hasa kupikia...

   

Na pia anao mbuzi...




Na hata kuku pia..   tena ni wazuri na wanono mno, yakhe...




Yaani kwa ujumla kila ninapofanya ziara nyumbani kwa huyu jamaa, huwa nainjoi sana. Wee acha tu!





No comments: