HOSPITALI YA SELIANI-ARUSHA

Hii ndio mandhari kidogo tu ya Hospitali hii ya Seliani; ipo katikati tu ya mji, jirani na maeneo ya Florida-Mjini Arusha).





Mojawapo ya magari ya kubebea wagonjwa ya hospitali hii likiwa limeegeshwa tayari kwa lolote.





Moja ya maeneo ya huduma kwa wagonjwa





Binti yangu akiwa amefanyiwa oparesheni ya tumbo katika hospitali hii ya Seliani 

Hapa mama yake pamoja na Shangazi yake wakijaribu kumbembeleza ainuke ili apate angalau chai; mwenyewe alikuwa hataki kabisa.






Aah, Wapi! Ametia mgomo kabisa.






Baadaye alikubali kunywa chai; na tabasamu likaonekana usoni pake. Akaamua apate picha kidogo na kaka yake; Bwana mkubwa Saadi.





Pamoja na matatizo ya binti yangu, lakini kama kawaida ndani ya hospitali yoyote ile kila mtu anakuwepo kwa ajili ya tatizo lake fulani linalomkabili. Kama familia hii ndani ya hospitali ya Seliani, ambayo ilijitambulisha kwa Mpini Wa Shoka kama familia ya Kisagase ya eneo la Unga Limited-Mjini Arusha, ambao walikuwa na hekaheka nzito na kitoto kichanga mno....

 Hapa wanahangaika ili kuhakikisha kinakunywa uji japo kidogo....

Wanafamilia wote wa Kisagase mjini Arusha Mpini Wa Shoka unawapeni poleni sana. Lakini maombi ya dhati kwa Muumba wa kitoto hiki ni muhimu sana, kuliko huzuni na unyonge mwingi usoni na moyoni. Pigeni nyoyo konde... hakuna linaloshindikana mbele zake.


No comments: