SABENA (IDARA YA MAJI)-ARUSHA TOWN


Mojawapo ya barabara za Jiji la Arusha zenye msongamano na hekaheka nyingi za magari na watu, mchana kutwa hadi giza la usiku linapoanza kuingia, basi ni barabara hii. Kwa wenyeji wa Jiji la Arusha, wanaifahamu zaidi kama barabara ya Sabena; ambapo pia kuna Ofisi za Idara ya Maji (Wizara), na hivyo pia kwa wengine wameizoea barabara hii kwa jina la Idara ya Maji. 

Msongamano mkubwa magari katika barabara hii, kwa sehemu kubwa huchangiwa na magari madogo ya usafiri wa abiria (daladala a.k.a Ais) yanayopeleka abiria maeneo ya Njiro, Kisongo, M'bauda, Majengo, Kwa Mromboo na hata Wilayani Monduli. Barabara hii ipo jirani kabisa na stendi ndogo ya daladala pamoja na ile ya mabasi makubwa yaendayo mikoani. Lakini pia kwenye barabara hii kuna maduka mengi ya vipuri (spea) vya magari ya kila aina, na hivyo kuwafanya watu wengi kufika hapa mara kwa mara,  kama unavyomwona huyo jomba hapo juu akiwa ameshikilia mkononi springi aliyoinunua punde.    


No comments: