URAFIKI WA PAKA NA BINADAMU HAUKUANZA JANA WALA LEO! NI WA ENZI NA ENZI, TANGU DUNIA HII ILIPOUMBWA NA MWENYEZI MUNGU.
Bi. Hawa Ramadhani, maarufu zaidi kwa jina la Mama Fatuma wa Mjini Arusha, akiwa mezani akipata msosi wa nguvu, shavuni akiwasiliana kwa simu; huku paka mzuri wa kupendeza akiwa amejilaza kwa pozi pembeni mwake. Kati ya moja ya tabia kubwa za mnyama huyu mdogo machachari anayeishi zaidi ndani ya nyumba za binadamu, ni kuchagua aina za vyakula anavyovipendelea zaidi. Ukitaka upatane na mnyama huyu, wewe mpe maziwa fresh, samaki wa kukaanga, dagaa na hata nyama ya kuchoma. Alooooh! Nakwambia hapo utakuwa umemnasa kwelikweli katika urafiki wenu. Lakini kama mezani kwako unakula ugali na mboga za majani, basi ujue kabisa wewe na paka siku hiyo urafiki wenu ni wa kubahatisha tu. Na hata kama akikubali kula hizo mboga zako za majani, ujue ni njaa tu ndio imemkamata vilivyo; kwa hivyo, hana namna nyingine ya kufanya! Au kama vipi, aamue kwenda zake kupanda juu ya dali la nyumba akajiwindie panya!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment