Kwa Mfano: "Unajiandaa Hivi Karibuni Kutoka Popote Pale Ulipo Hapa Duniani ili Usafiri (pamoja na familia yako kama unayo) Uende Ukawasalimie Wazazi Wako; Na Hili Hapa Chini Ndilo Daraja Pekee Linalotegemewa Kwenye Barabara Kuu Inayoelekea Huko Nyumbani Kwenu (HomeLand a.k.a Kijijini) Wanakoishi Wazazi Wako Pamoja Na Ndugu Na Jamaa Zako Wengine; Je, Kwa Hali Hii Bado Unao Huo Mpango Wa Kusafiri Kwenda Huko Kwa Wazazi Wako Kwa Kupitia Kwenye Daraja Hili..?


Hapa ni katika eneo maarufu linalojulikana kwa jina la Korongotatu, kwenye barabara Kuu ya Arusha-Simanjiro hadi Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara-Tanzania. Nguvu ya Maji imelivuruga vilivyo daraja hili muhimu, ambapo maji yamesomba hadi vyuma vya juu pembeni mwa daraja na kuyamegua kabisa mawe yaliyojengewa vema kwa sementi! (kulia.) Huduma juu ya Daraja hili ikawa imesitishwa kwa muda; magari pamoja na vyombo vingine vya moto vikawa havina namna, zaidi ya kutumbukia ndani ya Korongo lenyewe na kuendelea na safari zao!

Maji yakiamua kuleta balaa, ni hatari tupu Wakwetu...

No comments: