...Haya Ni Ya Udongo Wa Asili. Yanapochomwa Kwa Moto Yanabadilika Jina Na Kuitwa MATOFALI YA KUCHOMA.


Hapa yakiwa yameanikwa juani ili yakauke vema tayari kwa kupangwa kitaalamu kwenye tanuri la moto la kuyachomea. Hapa yalipo, adui mkubwa ni endapo mvua 'itaanguka' kwa ghafla! Yote haya yanaharibika kabisa. Yanayoonekana kwa nyuma, ni yaliyokwishachomwa lakini 'hayakuiva' vema; kwa hivyo yatachomwa tena ili yaive kwa kiwango na ubora unaohitajika. 




...baada ya kuwa yameiva vema kwenye tanuru, yanapanguliwa kwa utaratibu maalumu kwa ajili ya kwenda kuyatumia kwa ujenzi. Yaliyoiva vema yanakuwa na rangi ya kuvutia kama hayo yaliyo jirani na huyo aliyeinama mwenye shati la rangi nyeupe. Ambayo hayakuiva vema yanarejewa kuchomwa. Inaelezwa kuwa ubora na uimara wa matofali haya katika ujenzi ni wastani wa kudumu kwa miaka 100 hadi 150. Bei yake kwa saizi ya ukubwa huu kwa Mji wa Arusha, kwa sasa inazungukia Tshs 300/- kwa tofali moja. Hapa ni maeneo ya KwaMromboo. Kazi ni kwako... 

No comments: