ARUSHA-MCHANA
Ni mchana kweupeeeee, kijua kinawaka vema; kila mtu na harakati zake... Kila mtu na mipango yake.... kila mtu na mwelekeo wake kichwani. Ilimradi, kila mmojawao jioni inapoingia, basi ndipo anaanza kuhesabu alichokifanikisha kwa mchana mzima. Hapa ni maeneo ya katikati ya mji wa Arusha. Mnara wa kumbukumbu ya Azimio la Arusha unaonekana vizuri. Wewe unalikumbuka vema Azimio hili lilihusu kitu gani hasa? Au na wewe pia ni kama mimi tu! Hakuna lolote unalolijua kichwani, ilimradi jua linajichomozea tu asubuhi mashariki na jioni linajizamia zake taratibu magharibi, kwisha! Hebu umiza kidogo kichwa ulikumbuke Azimio hili la Arusha lilikuwa ni kwa ajili ya jambo gani hasa. Na hilo jambo lenyewe hadi leo bado lipo? Na kama halipo, sasa huu mnara unaendelea kukaa hapa kwa ajili ya kumbukumbu gani tena, wakati jambo lenyewe limebakia midomoni na kwenye makaratasi tu maofisini! Limejifia!
No comments:
Post a Comment