BURUDANI ZA KUKATA NA SHOKA ZIKAJA!


 Zilikuwepo burudani nyingi kutoka kwa wanafunzi wa madarasa mbalimbali. Lakini moja ya burudani zilizowasisimua wengi ni pamoja na igizo hili lililochezwa na watoto hawa kama mume na mke, ambapo mume ni cha pombe kupitiliza (mlevi komba) asiyeijali kamwe familia yake, hasa kielimu. Ilikuwa tamu kwelikweli.


Moreen Mlagala wa darasa la 4 (kushoto) na mwenzake aliyeshika kinasa sauti, wao walishiriki kama maafande waliomkamata baba huyu mlevi akiwa bwiiii mitaani na chupa yake ya gongo mkononi na kumsweka korokoroni! Ulevi ni noma! Ulevi ni soo! Ulevi ni balaa!

 

HALAFU....

Likaibuka hili kundi!  Sijui ni kutoka Sauzi kwa Mzee Madiba! Au ni kutoka Botswana kwa wazee wa Makirikiri! Weee! Acha tu. Ilikuwa ni hatari tupu, lakini salama! Ni wanafunzi hao wa Nalopa.



 

Kisha...

Ngonjera nayo ikatikisa.

 Hapa, siyo kwamba anatembea na mistari ya bongo fleva au Bongo HipHop! La hasha. Ni mambo ya mpashano tu wa maneno. Faidha Kassim wa darasa la 4 akitema cheche mbele ya mgeni rasmi pamoja na wenzake wa kikundi cha Ngonjera.

DJ in full mixing, naye hakuwa mbali na kasi ya mambo.

No comments: