Swahiba, Gerald Williams Chegenya akiwa amepozi kwenye Bodaboda yake katika kijiji cha Terrat wilayani Simanjiro mkoani Manyara tayari kwa kupeleka abiria katika vijiji vya jirani. Usafiri wa Bodaboda kwa sasa umekuwa ni miongoni mwa huduma za haraka mno kwenda katika sehemu moja hadi nyingine, na umetoa ajira kwa vijana wengi, na hata kwa watu wazima pia, mijini na vijijini, ingawa huduma hii kwa upande mwingine imekuwa ni tishio kubwa kutokana na ajali nyingi zinazotokea kila kukicha, kwa sababu wengi wanaojiingiza katika ajira hii hawana ujuzi wa kutosha, na pia mwendo kasi. Take care, USALAMA WAKO KWANZA, MAMBO YA HAKI BAADAYE.
|
No comments:
Post a Comment