MAMBO YA BIASHARA.
Maisha ni popote! Kambi ni kokote! Hebu tazama vizuri, wakwetu! Hakuna hata kimoja kinachokuvutia! Hakuna saizi yako hapa! Biashara ya viatu, hatua kadhaa tu kutoka soko kuu la Arusha. Mbele ya biashara hii, bango linaonesha barabara imefungwa. Ni kweli, barabara imefungwa; Wachina wamekwishavamia na kwenye kamtaa haka kafupi mno (mtaa wa Masai) kanakounganisha soko kuu na barabara ya Sokoine (Arusha-Dodoma road). Aina hii ya viatu (raba; enzi zake zikiitwa la kuchumpa) zimeondokea kupendwa zaidi na vijana wengi, hasa wa kiume, mkoani Arusha. Na wewe je, hazikufai kwa kuvalia na suti yako ya harusi!
No comments:
Post a Comment