Ni miongoni mwa maeneo yanayokuwa kwa kasi mno. Eneo la Kwa Mrombo lipo wastani wa Km 7 hivi kutoka katikati ya Mji wa Arusha, kwenye barabara kuu ya Arusha-Kiteto kupitia makao makuu ya wilaya ya Simanjiro; Orkesumet. Hapa kwa kawaida ni hekaheka na pilikapilika tupu, za kila aina, kwa mambo ya biashara ndogondogo na usafiri wa hapa na pale, bila kusahau nyama choma na ugali mkubwa. Kwa ufupi, pamechangamka mno.
|
No comments:
Post a Comment