MJINI, KUSHANGAA MUHIMU.
Hapa
ni dakika chache tu baada ya kutokea tukio la wizi kwenye moja ya maduka
yaliyopo katika mtaa huu mfupi unaoelekea Soko kuu (ukipitia kwenye tawi jipya
la NMB-Arusha). Mkusanyiko huu haukuja kirahisi hivi. Kwanza wote hawa
unaowaona, na wengine wengi tu usiyowaona kwenye picha, walitawanyika hovyo
huku na kule mfano wa vifaranga vya kuku visivyokuwa na mama, baada milio
kadhaa ya risasi za waporaji ndani ya duka hilo kurindima hewani. Waporaji
walifanikiwa kupora kiasi cha pesa na kutoweka. Hapa sasa ikabaki kila mmoja na
la kwake mdomoni! Mwingine simu sikioni akipeleka habari! Mwingine akijifanya
yeye ndiye aliyeona vema kila kitu! Ilimradi hapa, kila mmoja sasa alikuwa na
la kwake kinywani! Mpini Wa Shoka nao haukukosekana! Ilikuwa ni kama majira ya saa
kumi kasoro hivi ya alasiri.
No comments:
Post a Comment