WAKATI WA KUJINAFASI ULIPOFIKA.....



  Sahani mkononi, jicho kwenye madikodiko! Mimi nataka paja! Usiniwekee kipapatio naweza kuota mabawa kama kuku! Wazazi na waalikwa wote wakajimwaga kwenye mambo ya kumenyuka msosi.

 Vile vijianafunzi vidogovidogo navyo havikuwa nyuma katika kuyashughulisha meno!

 

Aaa! Kaka Saadi! Tonge kubwa sana? Au ndio utamu wa vitu umekuingia hadi unafumba macho! 

 

 Wale wavivu wa kula nao hawakuachwa wale wenyewe. Mwalimu Tumaini akimsaidia Shadya Jigge kumega mnofu wa kuku na kumlisha! Hongera mwalimu kwa upendo wako.


Wahitimu wa darasa la saba nao wakakaa kwenye darasa moja maalumu pamoja na wazazi, walezi na wageni wao; kazi ya kupiga msosi ikaendelea kwa kasi.

No comments: