CCM NAO HAWA HAPA NDANI HEKAHEKA KATIKA MOJA YA MIKUTANO YAO YA KAMPENI...


"Najiandaa kuelekea kwenye kampeni za chama changu." Mmoja wa vijana wa CCM akipeperusha bendera kubwa ya chama chake.


                                     Bendera kila upande wa gari.



Idadi ya waliohudhuria nayo ilikuwa ni kubwa ndani ya sare za chama


 Vijana wa kada na nafasi mbalimbali ndani ya chama nao hawakubaki nyuma katika kusema chochote walichokihisi ni muhimu ndani ya viwanja vya kampeni, kabla ya kuanza kumnadi mgombea wao.



Wapiga picha na waandishi nao walijitahidi kuchukua hiki ama kile; wengine wakiwa ni wale wa chama, kama huyu aliye ndani ya sare.



 Mgombea wao kwa nafasi ya udiwani Bwana Philip Mushi (anayecheka), akinadiwa jukwaani kwa kishindo mbele ya wapiga kura.



Mgombea mwenyewe kwa nafasi ya udiwani Bwana Philip Mushi akimwaga sera za chama chake jukwaani baada ya kunadiwa.



Wana-CCM wakimfuatilia kwa makini mgombea wao wakati akitamba jukwaani akimwaga sera kwa wapiga kura. Mwenye kofia nyeupe katikati ni mwenyekiti wa mtaa wa Jamhuri (Jaluo) katika kata hii ya daraja mbili, Mzee Husseni Dudu.

No comments: