HAKUNA KAZI ISIYOKUWA NA MAPUMZIKO JAPO KIDOGO YAKHE!

Kwenye gereji hii iliyopo eneo la Unga limited mjini Arusha, Mpini Wa Shoka huwa unapendelea sana kufika mahali hapa mara kwa mara kwa shughuli zake mbili 3. Ndipo kama bahati tu nikawanasa mafundi hawa wakiwa wamejipumzisha kidogo. Ulikuwa ni muda wa mchana, kijua kikiwa kimekubali kwelikweli...

Sasa sijui kama walikuwa wameamua kujipumzisha baada ya kupiga kazi nzito tangu asubuhi, au siku hii kazi za ufundi ndani ya gereji hii ndizo hazikuwa nyingi za kuwabana kwa saaaaaaaaaana kivile...!

 

Hapa ni mchanganyiko wa mafundi wa umeme wa magari, ufundi wa injini na hata kupiga rangi magari. Kumbe siyo kila fundi unayemwona kwenye gereji yoyote ile, basi ni fundi wa kila kitu! Kila mmoja ana ujuzi wake, japo wapo wenye ujuzi zaidi ya mmoja. Na hapa kilichonivutia zaidi, ni mchanganyiko wa umri (rika). Kwenye gereji hii wapo watuwazima, lakini pia wapo vijana wadogowadogo mno kama hawa unaowaona kwenye picha hii..





Wakati wakiwa wamejipumzisha, mara akafika huyu jamaa kushoto (mmoja wa mafundi wakongwe), Jackson Laizer 'Fundi Kipara' akaanza kuwatania hapa na pale. Basi ikawa ni burudani tu. Yaani kazi siyo lazima kununa na kukaza mimacho muda wote tu. Wakati mwingine unatabasamu kidogo. Aliyesimama pembeni ya Jackson Laizer 'Fundi Kipara' ni Abel Joseph a.k.a The Dimpoz. Waliokaa kutoka kushoto ni Sebastian Silas a.k.a KakiNane, Cilas Francis a.k.a Mwana (mwenye kofia), Peter Greyson a.k.a Shati na Estomii Lucas a.k.a Baloteli. Aisee! Ni Baloteli wa ukweli, au ni mauzauza tu?




Mojawapo ya zana za kazi ndani ya gereji hii. Kompresa ya upepo kwa kazi ya rangi za magari.




Hapa kuna zana mbili. Chuma kinene kilichosimama wima hapa jirani, ni mtambo wa kukunjia na kunyooshea vitu vigumu, hasa vyuma. Na kwa nyuma yake (yenye rangi ya bluu), ni mashine ya kuchomelea vyuma (welding)




Moja ya magari yanayoendelea kunyooshwa na kupigwa rangi ndani ya gereji hii.




Peter Greyson a.k.a Shati akiwa ameegemea kwenye mlango wa gari (daladala a.k.a Ais), akisubiri maelekezo kutoka kwa mwenzake, Abel Joseph a.k.a The Dimpoz, aliyelala chini ya uvungu wa gari na zana zake za kazi, walipokuwa wakilirekebisha gari hili.




Abel Joseph a.k.a The Dimpoz, in Action chini ya uvungu hadi kieleweke, na gari hili liondoke zake likiwa shwari kabisa...



No comments: