OLELE, MASHATI-ROMBO-KILIMANJARO

Wakati unapoingia ndanindani kwenye maeneo ya wenyeji wa hapa, utavutiwa mno na hali yake ya uoto wa asili pamoja na ule wa kupandwa na wanadamu... 


Hili ni shamba lenye mchanganyiko wa mazao. Hapa kuna mihogo, migomba, maharagwe na hata miti. Ni shamba lililoshibishwa vema mazao, kiasi cha kufanana kabisa na msitu fulani hivi ulioko mbugani!




Hata makazi na nyumba za wenyeji zinaonekana kwa shida mno, kutokana na kuzingirwa vilivyo na msitu wa mazao na miti ya aina mbalimbali, na hasa migomba.




Hapa ni mchanganyiko wa migomba, mikahawa (kahawa) na magimbi. Wewe unapenda kipi kati ya mazao haya matatu?




Mpini Wa Shoka uliikuta 'gari' ya mkulima (baiskeli) ikiwa imeegeshwa ndani ya shamba hili. Hapa kuna mchanganyiko wa migomba, maharagwe, magimbi, miwa na miti.




Kwa harakaharaka, unaweza ukahisi kwamba mama huyu anayeonekana kwa mbali kidogo, atakuwa anatembea ndani ya eneo lenye msitu mkubwa na wa kutisha mno. Na hata unaweza kumuwazia kwamba mbona anayahatarisha bure tu maisha yake kirahisirahisi namna hii, kwani hapa anaweza hata akavamiwa ghafla na wanyamapori wakali kama Simba au Chui, na kumraruararua vipandevipande! Aah, wapi, wakwetu! Humu, ndani ya msitu huu anamopita mwanamama huyu pamejaa nyumba nyingi tu za wenyeji (wakazi wa Olele). Na wala hakuna hatari yoyote ile inayoweza kumkuta kirahisi! Ni msitu wa mazao mchanganyiko pamoja na miti ya asili na ile ya kupandwa. 




Pamoja na mazao mengine yote yanayolimwa na kustawi vema hapa, lakini 'msosi mkuu' (chakula kikuu) cha wakazi wa eneo hili, kama ilivyo pia kwa maeneo mengine mengi tu ya mkoa wa Kilimanjaro, ni ndisi msee wangu. Ouh! Sorry. Ni ndizi. Unauona huu mkungu ulivyopendeza vema kwenye huu mgomba? Kama unaweza, basi nakuruhusu harakaharaka bila ya kuchelewa uchume vichane vyako viwili tu kabla ya mwenye shamba hajafika!

 

 

 Aisee, na wewe pia U're welcome kwa saaaaaana hapa Olele, Mashati-Rombo, uje ule mchemsho wa 'ndisi' baba'angu!  'I mean' ndizi bhwana.  

No comments: