UBUNIFU MWINGINE NI HATARI TUPU!

 

 Kwa mimi nilipokiona kwa mara ya kwanza kitu hiki kwenye karakana fulani ya vijana wa ufundi seremala wa mjini Arusha, hisia zangu ziliamini kabisa hii ni lazima tu itakuwa ni meza ya kuvalia na kubadilishia mavazi na mapambo chumbani a.k.a ya kujipodolea (dressing table), na hasa kwa akina mama. Lakini nilipojaribu kumhoji mmoja wa vijana mafundi wa karakana hii, akazifanya hisia zangu zibaki njia panda! Akadai eti hiki ni kiti. Kama ni kweli, hebu wakwetu na wewe macho yako yajaribu kukikagua kwa makini kitu hiki, halafu ujipe jibu sahihi wewe mwenyewe kwamba hiki kitakuwa ni kiti cha aina gani hasa! Na kitakapokuwa kimekamilika, kitakuwa kinawekwa wapi hasa ndani ya nyumba! Sebuleni..? Chumbani..? Au jikoni...? 

                                         Ni kiti kwa ajili ya Mfalme!  


 

Kiti kina droo!!



No comments: