KABLA YA KUINGIA KAZINI NA CHOMBO CHETU, NI VEMA TUKAKIFANYIA KWANZA MAREKEBISHO YA MSINGI ILI TWENDE NA KURUDI SALAMA HUKO TUENDAKO. KINGA NI BORA, KULIKO TIBA!


Mmoja wa vijana wa kikosi-kazi cha ukusanyaji wa vyuma chakavu (screpa) katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha, James Joseph ‘Babuu’, akiwa katika harakati za kupiga spana kwenye mojawapo ya matairi ya gari lao la kazi akirekebisha, kabla hawajaingia mitaani kuanza kusaka na kukusanya vyuma chakavu na kuvifikisha kwenye kituo (ofisi) chao kilichopo eneo la mtaa wa Jamhuri katika kata ya Daraja Mbili-Arusha town.




Mwenyewe si unaliona gari letu la kazi jinsi lilivyotulia kikazi zaidi! Hapa umbeya hautakiwi hata kidogo. Ni kazi tu kwa kwenda mbeeeeeere




James Joseph ‘Babuu’ mwenye fulana ya rangi ya kijani akiwa amepozi na spana yake mkononi katika picha ya pamoja na mwenzake Shabani Saidi ‘Kisiga’, wakati wakiendelea kulifanyia ukaguzi na marekebisho madogomadogo gari lao waliloliegemea..




Dereva wa gari hili, Juma khamisi ‘Rido’ mwenye fulana nyeusi, naye pia hakukaa mbali saaaaaaaana na maeneo husika ya merekebisho ya gari…




Shabani Saidi ‘Kisiga’ akihakikisha rejeta inashiba vilivyo maji ya kutosha, ili huko waendako gari lisije likawaletea degedege na kifafa cha magari.

 

  

Mpini Wa Shoka unasema: “Ni vema kwa kila mwenye chombo cha usafiri kujitahidi kukifanyia ukaguzi japo mdogo tu chombo chake, kabla ya kutoka nacho kwenda mahali popote pale. Vinginevyo, kila siku kwako itakuwa ni kilio cha samaki; machozi yanakwenda na maji!

No comments: