NI KWELI WEWE NI FUNDI MTAALAMU; FUNDI MZURI. LAKINI USALAMA WA MACHO YAKO UNAUJALI KWELI, SWAHIBA?


Mpini Wa Shoka ulimnasa rafiki yangu huyu, Jackson Alves 'maarufu kama fundi Babuu', akiwa ndani ya eneo lake la kazi, kwenye gereji iliyopo eneo maarufu la Unga-Limited jijini Arusha akiwa katika hekaheka za kuichomelea pikipiki hii kwa welding katika sehemu zake kadhaa alizoelekezwa na mwenye pikipiki hii. Ni kweli Mpini Wa Shoka ulimkuta jamaa akijituma vilivyo katika kazi hii, lakini suala la usalama wako mbona haulijali Fundi Babuu, na hasa macho yako, endapo kama yatarukiwa na cheche za moto wakati ukiendelea kuchomelea?




Fundi Babuu in Action. Pikipiki inaimarishwa vilivyo kwa kuchomewa kwa welding kila mahali panapotakiwa kushughulikiwa, lakini usalama wako mbona uko hatarini hadi miguuni! Kazi ni tamu, lakini usalama wako ni muhimu zaidi. Kuwa makini.

1 comment:

Anonymous said...

kazi nzuri kaka napenda hii blog duh hapa nilikuwa nimechelewa kujua hii blog kwani natafutaga blog yenye habari na picha za Arusha zijaona kama hii blog zingine wanapiga picha bila yamaelezo wala kueleza hapo ni sehemu gani lakini wewe mwenye blog hii bigup leo ndio nimegundua hii blog kaza buti kazi nzuri sana endelea kutuletea habari za arusha haswa sisi wengine tuliondoka ARUSHA ziku nyingi tuko nje ya nchi piga picha maeneo ya sanawari kuanzia naura springs kuelekea moshi haswa pale darajani na mianzini