BIASHARA MTAANI


Huu ni mkaa wa kupikia. Ni biashara nzuri tu inapofika mijini kutoka maporini unakotayarishwa, ingawa kwa hakika ni biashara ya hatari mno kwa ustawi na uhifadhi wa misitu, hasa ile ya asili. Lakini hapa nataka uyachunguze kwa makini haya makopo kwenye picha hii. Ni kwamba muuzaji wa huu mkaa ameyaponda kwa makusudi haya makopo ili awaibie wanunuzi? Au haya makopo hivi ndivyo hasa yalivyo? Na wanunuzi wenyewe wanaridhika kabisa! Au macho ya kila mmojawao hayana ushirikiano mzuri wa kutosha wa kuliona hili kwa usahihi? Maisha ya mjini hatari, wakwetu!  

No comments: