HEBU JARIBU KUKADIRIA HAPA...!

Mpini Wa Shoka uliwafuma watoto hawa wakioneshana ustadi, uwezo na ufundi wa hali ya juu katika kusukuma 'chandimu' (mpira wa karatasi). Ni ndani ya Majengo ya Juu-jijini Arusha.... Yawezekana hata wakina Samuel Etoo Fils..! Victor Wanyama..! Alex Song..! Mbwana Samatta..! Michael Essien..! Christopher Katongo..! Nadir Haroub 'Canavaro'..! Haruna Niyonzima..! Juma Kaseja, na wengineo wengi maarufu..! nao pia walizianza harakati za safari zao za kisoka kama ilivyo kwa watoto hawa, kwenye viwanja na maeneo mfano wa haya, ambayo wakati mwingine hayavutii wala kupendeza kabisa....!    


Haya twende..! Lakini ni mpambano usiokuwa na mwamuzi. Ni akili kichwani mwako tu..!



Kazi ni moja tu. Hapigwi mtu chenga; na wala hapitwi mtu kirahisirahisi hapa... 



Ouh! Chini! Almanusura mmoja wa wachezaji apindukie kwenye makopo ya biashara ya mkaa, baada ya kukumbana na dhoruba kutoka kwa mmoja wa wachezaji wenzake. Sijui hata mwenye biashara hiyo ya mkaa angemfanya kitu gani hasa endapo angeyaangukia makopo yake! 



Anakwenda na mpira pale...! Anawatoka kwa ufundi...



Ajali nyingine kwenye uwanja uliojaa kila aina ya uchafu na takataka. Wenyewe wala hawajali chochote..



Shughuli ni nzito hadi kiatu kimemchomoka mguuni...



Kwa hisia zako tu, hebu jaribu kuwavua haya mavazi yao waliyoyavaa; halafu wewe uwavishe jezi na bukta za timu yoyote ile unayoipenda sana hapa duniani, kisha uniambie picha hii ya watoto hawa wa Majengo ya Juu-jijini Arusha ina tofauti gani na picha za mpambano mkali wa mojawapo ya mechi za ligi mojawapo kubwa kabisa duniani ya Mpira wa miguu? Nyota njema, huanza kuonekana asubuhi, Wakwetu... jioni mahesabu.

1 comment:

Anonymous said...

yaani nikiwaona watoto wanapenda michezo lakini wanakosa sehemu ya kuchezea naumia sana tanzania ni nchi yenye aridhi kubwa lakini kutengwa sehemu ya watoto kuchezea hiyo sera hakuna mafisadi changanya na rushwa watoto wanakosa haki yao ya msingi ya kucheza watoto wanazaliwa na vipaji lakini vinakufa kwa kukosa support inasikitisha sana vipaji vya watoto wetu vinakufa hivihivi tanzania yetu jamani