KALI YA LEO!


Haya maisha ndani ya hii dunia yana vituko na mikasa yake chungu nzima, Wakwetu! Pitapita za Mpini Wa Shoka ghafla ziligongana na kihoja cha huyu bwana braza-kaka, ambaye alikuwa ameyatwika maji vilivyo kichwani (amelewa). Sikuweza kubahatika kulinasa kirahisi jina lake, lakini jamaa alikuwa ameamua kuwagawia watoto pesa (baadhi ya watoto hao nyuma yake). Mgao wake ulikuwa ni wa Sarafu (Coins) tupu tu! Hakuna noti hata moja iliyotoka ndani ya mifuko yake! Wanaomfahamu vema walinidokeza kwamba hali ya maisha ya ndugu huyu ni ya kawaida mno; lakini akishalewa tu kama hivi, inaonekana huwa anajihisi yeye ndiye tajiri mkubwa na nambari one kuliko wote duniani! Ulevi ni noma..! Ulevi ni hatari, Wakwetu! Chunga sana. Hapa alikuwa akieleaelea tu kwenye mitaa ya Kata ya Daraja Mbili-jijini Arusha

No comments: