UKILA, NI LAZIMA ULIPE...


Katikati ya Mji wa Arusha, Mpini Wa Shoka ulikutana na sakata hili katika eneo la Makao Mapya-kwenye kimtaa hiki kidogo kilichopo ubavuni mwa msikiti wa Kuba (Masjid Kuba), mita chache tu kutoka mgahawa wa Cafe La Aziz, ambapo vijana wawili (wa kwanza kabisa kulia mwenye kofia ya mviringo aliyevalia koti na mwenzake mwenye fulana ya rangi nyeusi), walijikuta ndani ya mzozo mkali na watu kadhaa, baada ya kudaiwa kula chakula kwa Mama Lishe (Mama Ntilie) mmoja wa mtaa huu na kujaribu kutaka kutengeneza mazingira ya kihuni na kibabe ili wasilipe pesa za chakula. Patashika na mzozo mkali wa kuwabana walipe, ndio uliosababisha kikundi hiki kidogo cha watu kijazane kama kinavyoonekana. Walikubali kulipa kwa fujo nyingi! Nahisi haka katakuwa ni kajitabia kao ka kila mara katika maeneo kadhaa; wakisahau kwamba kwenye Ofisi za watu mjini Ukila chochote, ni lazima Ulipe! (Niwie radhi sana kwa mwonekano wa picha, kwani nilizinasa nikiwa nyuma ya kioo kwa mbali kidogo kutoka eneo la tukio).

No comments: