FUNDI, UNAJIPENDA KWELI, WEWE?


Eneo la Kwa Mromboo kwenye uwanja wa biashara ya nyama choma, Mpini Wa Shoka ulibahatika kumnasa fundi huyu akiwa na mwenzake wakiendelea na kazi ya kubandika vigae (tiles) kwenye ukuta. Walikuwa wakifanya kazi nzuri sana. Lakini kilicholivutia jicho la Mpini Wa Shoka ni namna ambavyo fundi huyu alivyokuwa ameamua kuuweka mwili wake katika mazingira ya hatari mno, kwa kuzitumia ndoo mbili kupanda juu yake akizifanya ndizo ngazi! Na cha hatari kabisa, ni jinsi hizo ndoo alivyozitegeshea kwa chini jiwe dogo la kumuwekea uwiano (balance) ili asiyumbe; jiwe ambalo limekaa kwenye ukingo kabisa wa ndoo (tazama kwa makini). Jamani! Wakwetu, hivi huyu fundi anaujali kweli usalama wa mwili wake?     


 

Hiki ndicho kibanda kipya (Ofisi) cha nyama choma, ambacho fundi huyu na mwenzake walikuwa wakikifanyia kazi... 

No comments: