SANAWARI PAMOJA NA MAENEO YAKE YA JIRANI-ARUSHA TOWN


Hii ni barabara ya East Africa. Huko chini anakotokea huyu jamaa aliyebeba kipochi, ni pande za kwenye majengo (Ofisi) ya E.A.C-East African Community pamoja na A.I.C.C-Arusha International Conference Centre (mkono wa kushoto kwenye msitu mkubwa wa miti pamoja na jengo la ghorofa linaloonekana kwa mbali). Na mkono wa kulia (anakoelekea huyo bwana mkubwa anayevuka barabara) ni upande wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Arusha-Mount Meru Hospital.




Hapa ni kwenye tuta (bams), magari yakitokea upande wa hospitali ya Mount Meru yakielekea kwenye mataa ya kuongozea magari (traffic lights) ya Sanawari.




Kwenye barabara hii ya East Africa; kabla ya kuyafikia mataa ya kuongozea magari ya Sanawari, utakutana na jengo hili kubwa la kuvutia lililonakshiwa vema kwa rangi ya bluu. Lipo jirani kabisa na mataa hayo. Hii ni hoteli maarufu Jijini Arusha; inaitwa Naura Springs. Siku hizi majengo marefu hata zaidi ya hili, yanaoteshwa kama uyoga kila pembe ya Jiji la Arusha  




Hapa ni nje ya lango Kuu (main gate) la kuingilia ndani ya hoteli ya Naura Springs (upande huo yalikoegeshwa magari mengi)




Tumewasili kwenye mataa ya kuongozea magari. Unayaona vema mbele yako? Hili gari jeusi linateremka kuelekea pande za AICC na Mount Meru hospital.




Hapa ndipo penye mataa. Gari la rangi ya kijani baada ya kuruhusiwa, nalo pia linateremka kuelekea pande za AICC na Mount Meru hospital likitokea pande za Dar au Moshi (Kilimanjaro). Hayo magari yanayonyoosha barabara moja kwa moja yanaelekea pande za Mianzini hadi Arusha katikati ya Mji.




Haya yanakuja kwa kasi baada ya mataa kuyaruhusu. Yanatokea pande za Dar au Moshi (Kilimanjaro)

 


Kwenye barabara hiyo upande yalikosimama magari pamoja na pikipiki, ndio barabara inayopanda kwenda Sanawari Juu. Zamani barabara hii ilikuwa ni finyu mno; wananchi walikuwa wamejenga majengo jirani kabisa na barabara hii. Lakini kwa sasa barabara hii imepanuliwa kwa kiwango cha kuvutia, japo bado ni barabara ya vumbi. Idadi kubwa ya majengo ilivunjwa ili kuupisha upanuzi huo. Siku hizi hata magari manne yanapishana kwa wakati mmoja, bila ya wasiwasi wowote ule. Ukitaka uzuri, ni lazima udhurike Wakwetu...




Tazama kwa makini. Hilo gari dogo la rangi nyeupe (pembeni mwa pikipiki) limekata kona likielekea pande za Sanawari ya Juu, baada ya taa (tazama juu kabisa ya picha hii) kuliruhusu lipite.



Hapa tupo kwenye msururu mrefu wa magari, jirani na hoteli ya Mount Meru, karibu kabisa na darajani (tazama mbele mkono wa kulia kwa makini) tukielekea kwenye mataa ya kuongozea magari ya Sanawari. Siku hizi hata Mji wa Arusha nao pia umekuwa na msongamano mkubwa wa magari, japo barabara nyingi zimefanyiwa matengenezo makubwa, na nyingine zimebuniwa (mpya)

2 comments:

Anonymous said...

ubarikiwe sana kwa picha hizi na maelekezo mazuri hakiki Arusha pamebadilika sana nafikiri nikirudi nyumbani nitapotea maana kwa sasa nakaa nje ya nchi tena hapo sanawari ulipoonyesha naishi karibu hapo nimefurahi sana wewe ni taalamu kweli maana wengine wanawekaga picha bila maelezo ya kutosha lakini wewe umemaliza kila kitu big it up brother napenda sana kutembelea blog yako kwani siku nyingi nilikuwa natafuta blog ambaye itatuabarisha habari za Arusha nilikuwa sijaona hii blog yako mapema kila siku lazima nikutembelee ktk blog yako endelea kutuabarisha God bless you

Anonymous said...

kazi nzuri lakini kuna sehemu umega picha zimekuwa na giza hazionekani vizuri sijui ni kamera yako au ulizipiga usiku shughulikia brother athorwise u do good job