DUKA JIPYA; KIJIJI CHA M'BUYUNI-ARUSHA VIJIJINI (ARUMERU).

Ni mwendo wa kama 38km hadi 39km kutoka Arusha mjini kwa kupitia barabara Kuu ya Arusha-Simanjiro-Kiteto (kupitia Mbauda), ndipo lilipo duka hili, pembezoni kabisa mwa barabara kwenye geti la kituo cha ukusanyaji wa ushuru katika kijiji cha M'buyuni-Kata ya Oljoro...  





 

Japo ni duka lililopo eneo la kijijini, lakini wahusika wamejitahidi sana kulipangilia vema...


Hivi ndivyo bidhaa na dawa za aina mbalimbali zilivyowekwa katika mpangilio, pamoja na bei zake kusomeka vema




Kijana Goodlucky Sikorei ndiye mhudumu (muuzaji) katika duka hili. Hapa, akiwa katika utaratibu wake wa kawaida wa kuweka mambo na mahesabu yake vizuri ndani ya madaftari, akiutimiza ule usemi wa 'mali bila daftari, hupotea bila ya habari.'

 

 

Wananchi wengi wa Kijiji cha M'buyuni na wa Kata nzima ya Oljoro kwa ujumla, wameonesha wazi kufurahishwa mno na kitendo cha kusogezewa (kuanzishwa) jirani kabisa na maeneo yao huduma ya duka hili, na hivyo kuwapunguzia mzigo wa kusafiri mara kwa mara kwenda Arusha mjini kununua dawa pamoja na bidhaa nyingine za kilimo na mifugo, ambazo kwa sehemu kubwa sasa zinapatikana ndani ya duka hili jipya kwa bei za kawaida tu.   



 

Haya Ndio Mandhari (mwonekano) ya Kijiji Cha M'buyuni, sehemu ya barabarani (barabara Kuu ya Arusha-Simanjiro-Kiteto), lilipo duka hili jipya la pembejeo za kilimo na mifugo...

Hili ni duka la kuuza dizeli na petroli ya kupima...




Wanakijiji na mazungumzo pembezoni mwa barabara....




M'buyuni Center (Madukani)



No comments: