Mpini Wa Shoka NDANI YA HOSPITALI YA WILAYA YA MERU-TENGERU, ARUSHA


Zamani ikiitwa hospitali ya Wilaya ya Arumeru. Baada ya Wilaya ya Arumeru kugawanywa mara mbili (kiserikali) na kupatikana Wilaya mpya za Arusha (Arusha Vijijini) na Meru, hospitali hii yenyewe ikabaki kuwa ni Hospitali Kuu ya Wilaya ya Meru. Mpini Wa Shoka umeshuhudia marekebisho na ukarabati mkubwa mno uliofanywa na Serikali wa kuiboresha hospitali hii katika maeneo na nyanja mbalimbali, na hasa majengo na wodi (wadi)...


Baada ya kuingia kwenye geti Kuu la Hospitali, hili ni geti la pili kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye mawodi (wadi). 




Majengo ya kuvutia ya madaktari...




 Vibao vya maelekezo na matangazo mbalimbali kwenye barabara ya kuelekea kwenye mawodi na kwa madaktari...




Ukiangalia kwa makini, mbele kabisa wanakoonekana watu, ndipo kwenye Geti Kuu la kuingilia kwenye hospitali hii. Geti la pili nalo pia linaonekana...





Upande wa huduma kutoka kwa madaktari pamoja na kliniki..



Magari ya hospitali yakiwemo ya kubebea wagonjwa.... 



Baadhi ya mawodi (Wadi). Wananchi wakielekea kuwajulia hali wagonjwa wao...



 

Hivi ndivyo ndani ya baadhi ya mawodi (wadi) palivyo....

 

Pamegawanywa vyumba vyenye kuingia vitanda viwiliviwili kwa kila chumba..




Katikati ya wodi kuna TV kubwa kwa ajili ya kuwaelimisha, kuwaburudisha na kuwahabarisha wagonjwa pamoja na wale wanaofika kuwaona...


No comments: