Vijana Wanaoishi Mazingira Magumu Wanapopata Upenyo Ndani Ya Ukumbi Wa Sherehe...



Ni usiku wa karibu saa tano hivi ndani ya jengo la C.C.M (Chama Cha Mapinduzi) Mkoa wa Arusha kwenye ukumbi uliokuwa ukifanyika shughuli ya harusi, Jicho la Mpini Wa Shoka lililinasa kundi la vijana hawa wanaoishi katika mazingira magumu-mitaani ndani ya Jiji la Arusha nao pia 'wakijimwaga' kwa raha zao...


Wakati wenzake 'wakijimwagua' katikati ya ukumbi, huyu yeye muda wote alikuwa akivuta kwa njia za pua na mdomo mafuta aina ya petroli yaliyochanganywa kwenye gundi ya kuunganishia soli za viatu, ambayo imo ndani ya kichupa alichokificha kwa ujanja ndani ya sweta lake...




 

Kijana 'amejiachia' vilivyo kwa burudani...




Mapozi makali ya picha mbele ya jicho la Mpini Wa Shoka....

 

 

'....lakini usisahau kwamba, hawa wanapokuwa wakubwa huwa wanahitaji kujitegemea ndani ya jamii. Miongoni mwao hugeuka kuwa ni watu hatari sana kama majambazi na wauaji. Ingawa pia wamo wanaokuja kuwa miongoni mwa watu wema sana. Tukiweza kuwajenga na kuwasaidia sasa, basi tusisite kufanya hivyo; maana wao pia ni binadamu kamili'

No comments: