KWA KWELI, HOJA ZINGINE NI UTATA MTUPU...!


Mwenye kikapu mkononi ni muuzaji wa karanga zilizokaangwa mitaani. Aliyeshika gari ni dereva wa teksi, Bw. Hashim. Na aliyekaa juu ya pikipiki ni dereva wa BodaBoda, Bw. Dosiani. Mpini wa Shoka uliwafuma vijana hawa wa Mji wa Arusha wakijadiliana juu ya hoja hii: "...eti, kwa ajili ya usafi wa unyoaji wa nywele katika maeneo mbalimbali ya mwili wa binadamu; Je, katika enzi hizo za zamani wakati ambapo nyembe, mikasi na visu vilikuwa bado havijagunduliwa, mwanadamu alikuwa akitumia kitu gani hasa kunyolea nywele zake? Na kama alikuwa hanyoi kabisa, inawezekana eti hicho ndicho chanzo hasa cha kugunduliwa kwa mavazi ya aina yake kama vile misuli na majoho ili kuhifadhi 'misitu' ya nywele zisizonyolewa? Na katika vile vipindi vya joto, hali ya hewa ya miili yao ilikuwa vipi katika suala zima la harufu kali?

No comments: