Eti Wanasema kwamba "Siku Hizi Uchakachuaji Katika Kila Kitu Ndio Mwendo Halisi Wa Maisha Ya Dunia Hii Tunamoishi...!

 

Hiki ni Kiwanda Kidogo Cha Ufyatuaji Wa Matofali, Eneo La UngaLimited Jirani Kabisa Na Shule Ya Sekondari Ya Sinoni-Jijini Arusha...

 Viwanda vya aina ni vingi mno katika maeneo mbalimbali ya nchi. Je, ni nani hasa mwenye jukumu la kuhakikisha uimara na ubora wa bidhaa zake kabla mnunuzi hajaenda kuzitumia? 

  

Tofali zikikauka juani baada ya kufyatuliwa... Ni tofali zilizotengenezwa kwa mchanganyiko wa sementi, mchanga na moram. Eti, Huenda Hata Haya Nayo Pia Yatakuwa Yamekwishachakachuliwa...!




Hapa zikiwa tayari kwa kuuzwa... Pembeni yake, kifusi cha moramu nyeupe kwa ajili ya kazi.




Vijana wakiwajibika vilivyo katika uchanganyaji wa malighafi ndani ya mashine ya uchanganyaji (ya mviringo) inayoendeshwa kwa nguvu za umeme...





Kisima kidogo cha akiba ya maji. Wakati Wote Kazi hii ya ufyatuaji wa matofali huwa inahitaji sana uwepo wa maji, tena ni maji ya kutosha kwa kipindi chote cha kazi...




Baada ya kufyatuliwa, vijana huzipanga vema kwa ajili ya kukauka...


No comments: