 Ni wakati wa maandalizi. Hapa ulikuwa ni mpambano wa kuvuta kamba kati ya vijana wa msikiti wa Taqwa na wale wa msikiti wa majirani zao; Masjid Mun'nawara (msikiti wa kwa Mzee Rajabu)
Ni wakati wa maandalizi. Hapa ulikuwa ni mpambano wa kuvuta kamba kati ya vijana wa msikiti wa Taqwa na wale wa msikiti wa majirani zao; Masjid Mun'nawara (msikiti wa kwa Mzee Rajabu)  Mashabiki na washangiliaji walikuwa wamefurika kila upande wakishuhudia...
Mashabiki na washangiliaji walikuwa wamefurika kila upande wakishuhudia...  Matayarisho na uhakiki wa waandaaji bado unaendelea ili kuuthibitisha ubora wa kamba....
Matayarisho na uhakiki wa waandaaji bado unaendelea ili kuuthibitisha ubora wa kamba....  Wakina mama na watoto nao pia walikuwepo tele...
Wakina mama na watoto nao pia walikuwepo tele...  Haya sasa! Mambo yameiva. Jamani, timu zote mbili mko tayari... "Ndiyooooooo, tuko tayari". Haya kila mmoja aikamate vema kamba.... moja! Mbili! Tatu.....
Haya sasa! Mambo yameiva. Jamani, timu zote mbili mko tayari... "Ndiyooooooo, tuko tayari". Haya kila mmoja aikamate vema kamba.... moja! Mbili! Tatu.....   ...haya twende! Vuta! Vuta! Nikuvute!
...haya twende! Vuta! Vuta! Nikuvute!  Ustaadh acha kutegea. Umoja ni nguvu. Vuta! Kazana! Kazana! Vuta nikuvute... Ooooop!
Ustaadh acha kutegea. Umoja ni nguvu. Vuta! Kazana! Kazana! Vuta nikuvute... Ooooop!  Mwamuzi katikati (mwenye kanzu na kilemba) anainua mikono juu kuashiria tayari mshindi amepatikana.... Ndiyo! Mshindi amepatikana....
Mwamuzi katikati (mwenye kanzu na kilemba) anainua mikono juu kuashiria tayari mshindi amepatikana.... Ndiyo! Mshindi amepatikana....  Mikono juu ikishangilia ushindi. Vijana wa Masjid Mun'nawara (msikiti wa kwa Mzee Rajabu) ndio washindi kwa kuishinda timu ya vijana wa msikiti wa Taqwa. Ilikuwa ni vuta nikuvute tamu na ya aina yake...
Mikono juu ikishangilia ushindi. Vijana wa Masjid Mun'nawara (msikiti wa kwa Mzee Rajabu) ndio washindi kwa kuishinda timu ya vijana wa msikiti wa Taqwa. Ilikuwa ni vuta nikuvute tamu na ya aina yake...
No comments:
Post a Comment