Ni
utitiri wa watoto, wakubwa kwa wadogo, kutoka pande mbalimbali za vitongoji na mitaa kadhaa ya Mji wa
Arusha wakiwa wamejumuika pamoja katika kituo hiki cha michezo....
Hawa wakiwa katika mchezo wa mabembea...
Wengine wakiwa ndani ya Helkopta! Mambo ni juu kwa juu, mwanawane....
...hawa wao walikuwa katika kuendesha farasi.
Hii ndio ilikuwa kali kuliko. Hapa hata namna ya kuchukua picha ilikuwa ni kazi. Hili dude lilikuwa limejaa watoto kibao! Halafu lilipowashwa lilikuwa linakwenda kasi siyo mchezo. Picha yenyewe si unaona jinsi nilivyoinasa kwa tabu! Yaani jinsi lilivyokuwa likizunguka, kwa watoto kwao ilikuwa ni raha tupu...
No comments:
Post a Comment