KWA HAKIKA, siri ya ardhi ya hii dunia tunayoringia ni yeye mwenyewe aliyeiumba ndiye anayeijua. Wala kamwe asikudanganye mwanadamu yeyote yule, hata kama ni profesa au mwanasayansi aliyebobea! Aisee, usilale na kuamka tu burebure kila siku bila ya kumshukuru na kumnyenyekea Muumba wako! Hebu tazama hili balaa ndipo utakaponielewa vema.... hapa ni ndani ya The United States of America, kwa werevu na wajuzi..!



Nyumba hii  imesambaratishwa na nyingine 27 zimehamwa haraka na wakazi wake, kufuatia maporomoko ya ardhi mapema siku ya Jumanne katika eneo la North Salt Lake-Utah nchini Marekani. Kwa mujibu wa ofisa mkuu wa kitengo cha moto wa eneo hilo, Bw. Jeff Bassett, kumekuwa na hofu kubwa kutokana na kuzidi kwa hali hiyo ya ardhi ya kumomonyoka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. 

Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa za mtu yeyote yule aliyejeruhiwa...




Unaziona nyumba jinsi zilivyo za 'nguvu kwelikweli', lakini hapa ardhi yote imetepeta kabisa kwa maji. Inamomonyoka ovyo tu yenyewe kama unavyoliona hilo eneo la katikati lilivyomomonyoka kama vile kuna mgodi wa machimbo ya kokoto...

 



Huyu ni mmoja wa wakazi wa nyumba za eneo hili, Bw. Lo Nestman, akiamua kuikimbia nyumba yake namba 761 ili kujiepusha na balaa la kuangukiwa. Vyepesi vya kuhama navyo kwa haraka ni kama haya mabegi. hapa hakuna ujanja wa kuhama na kabati. Kwanza kuokoa roho; halafu mambo mengine baadaye...  




Roho mkononi! Bibi amekurupuka kutoka ndani bila hata ya viatu miguuni! Unafanya mchezo na hatari wewe! "Dakika yoyote ile nyumba inaweza ikapiga mweleka, hebu nihamisheni haraka," ni kama vile bibi huyu anawasisitiza waliomshika... Poleni sana wakazi wa Utah.

"Unaweza ukalala ni tajiri, ukaamka ni mkimbizi kwenye nyumba ya jirani..!"

No comments: