MAFURIKO-MTWARA!

Mpini Wa Shoka leo uko Mtwara. Wakati nikijiandaa kutaka kukumalizia picha nyingine zaidi na zaidi za safari yangu ya Arusha-Dar (Dar es salaam), kabla ya kukupa za sehemu nyingine ya safari yangu, leo mapema asubuhi nikitokea Dar nikafika Mtwara kwenye saa 11 hivi ya jioni. Kabla hata sijapata muda mzuri wa kuvinjari katika mitaa ya Mji huu wa Mtwara, mara mwenyeji wangu Bwana Swallah Saidi wa MtuKwao Community akanipa taarifa ya kusikitisha kidogo. Wakazi wa nyumba zipatazo 100 wa eneo la Kiyangu mjini Mtwara, mapambazuko ya asubuhi ya leo yamewakuta katika wakati mgumu mno, baada ya nyumba zao kuzingirwa kila upande na mafuriko ya maji ya mvua iliyonyesha usiku, kiasi cha kuwafanya karibu wote kushindwa kutoka na kuelekea katika maeneo yao ya kazi. Bwana Swallah aliyenipeleka katika eneo hili, ambapo naye pia ni mmoja wa wakazi wa eneo hili anasema, yeye alifanikiwa kutoka na kuelekea ofisini mnamo saa 7 ya mchana! Sehemu kubwa ya nyumba hapa, maji yalivamia sebuleni hadi vyumbani na kusababisha tafrani na hekaheka kubwa ya kuokoa vitu mbalimbali huku na kule. Hakuna taarifa za mtu hata mmoja aliyekufa.....  

Hata wenye biashara hawakuweza kabisa kuzifungua!








 

Wa kule wakae hukohuko waliko, na wa huku tukae hukuhuku tuliko hadi siku maji haya yatakapoamua kukauka! Na je kama mvua zitaendelea kunyesha zaidi, itakuwaje! Wakwetu, mbona tutakimbia kabisa!





Kama unataka kutoka kwenda mahali fulani, basi unatakiwa uende kwa miondoko kama ya huyu jamaa hapa chini! 

Poleni sana wakazi wa Kiyangu.

 


No comments: