SEMINA-MTWARA.
Hii ni semina ya siku moja iliyofanyika siku ya J'mosi 05/01/2013 kwenye ukumbi uliopo katika jengo la kampuni ya simu Tanzania (T.T.C.L) mjini Mtwara. Lengo la semina hii lilikuwa ni kuangalia matokeo ya kuwepo kwa redio za jamii nchini Tanzania na changamoto zinazozikabili, pamoja na jukumu lililonalo mashirika na asasi za kiraia nchini. Semina hii iliandaliwa na shirika la MtuKwao (Mtukwao
Community Media) la mjini Mtwara, ambalo hivi karibuni linatarajiwa kuanza rasmi matangazo ya redio kupitia redio yao itakayosikika hewani kwa jina la Jamii FM katika mikoa ya Mtwara na Lindi.... Mpini Wa Shoka nao ulikuwemo.
Hawa ni washiriki kutoka Mtukwao
Community Media. Miongoni mwao ni Issa Hemed (wa kwanza kushoto) ambaye pia ni mmiliki wa blog ya Mtwaraone, na Bi Hajra aliyejitanda mwisho kulia. Hawa ni sehemu tu ya wale wanaotarajiwa kuwa watangazaji, watayarishaji wa vipindi na habari pamoja na wataalamu wa masuala mengine ndani ya Jamii FM-Mtwara itakapoanza rasmi kurusha matangazo yake.
Sehemu ya washiriki kutoka asasi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na klabu ya waandishi wa habari Mtwara.
Mmoja wa wawezeshaji Bwana Swallah Saidi kutoka Mtukwao
Community Media akisisitiza jambo mbele ya washiriki. Aliyekaa pembeni yake ni mwezeshaji mwingine Bwana Bright Msalya.
Wakati wa mapumziko mafupi, washiriki wakitoka nje ya ukumbi kwa muda ili kupata chochote kwa tumbo.
Sehemu ya washiriki wengine kutoka asasi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (waliokaa mbele). Wanaoonekana nyuma yao ni Muddy na Shafii wa Mtukwao
Community Media (Jamii FM-Mtwara).
No comments:
Post a Comment