MTWARA TOWN.

Pamoja na adha kubwa ya hali ya mvua zilizoleta kizaazaa kikubwa kwa sehemu ya wakazi wa Mji wa Mtwara kunasa kwenye mafuriko baada ya nyumba pamoja na magari yao kuzingilwa na maji kila upande kwa siku kadhaa sasa. Lakini siyo vibaya nikakupitisha hata katika maeneo machache tu ya Mji huu wa Mtwara.


Unapokuwa ukianza kuwasili katika Mji wa Mtwara kwa barabara ya Dar-Lindi-Mtwara, utapokelewa kwanza na ufukwe mpaka wa maji ya bahari ya Hindi.



Hapa ni maeneo ya Bima. Panaonekana mmojawapo wa minara ya kumbukumbu ya mashujaa wa mapambano ya ukombozi wa Msumbiji.

 

  

Hii ni barabara ndefu iliyonyooka kwelikweli ikitokea Dar-Lindi-Mtwara. Na kwa Mtwara Mjini inapitia Bima, Posta, Bodi ya Korosho hadi kanisa Kuu Katoliki-Mtwara (upande huu inakokuja bodaboda inayofuatwa nyuma na Bajaji), ikikutana na barabara kubwa ya kuelekea Bandari kuu ya Mtwara.

 

 

Hili jengo linajieleza vema lenyewe.





Chuo Kikuu kilichopo mkabala na jengo la Kanisa Katoliki Mtwara. Sehemu ya majengo ya Chuo hiki Kikuu katika picha ya chini...






Kanisa kuu Katoliki Mjini Mtwara. 

 

No comments: